Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amefanya Ziara ya kikazi kwenye Chanzo cha maji cha Ihelele,Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kinachosimamiwa na kuendeshwa na mamlaka ya KASHWASA.

Chanzo cha Ihelele ni chanzo pekee cha skimu ya maji kutoka ziwa Victoria inayohudumia mikoa sita ikiwa ni pamoja na Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Tabora na Singida.

Aidha chanzo hiki kinapeleka maji katika Mamlaka za Maji nane(8)ambazo ni: SHUWASA,KUWASA,MAGAWASA,KIWASA,TUWASA,NZUWASA,IGUNGA na MWAUWSA-NGUDU.Vilevile Vyombo vya watoa huduma ya majisafi ngazi ya jamii(CBWSO) zipatazo 95 na Migodi 3,inapata huduma ya maji kupitia Skimu hii. 

Mhe.Aweso akitoa maelekezo kwa Wakurugenzi na Menejimenti za Mamlaka za maji katika Ukumbi wa mkutano wa Ihelele.

Mkurugezi Mtendaji wa KASHWASA Mha.Patrick Nzamba akielezea namna ya shughuli mbali mbali za  uendeshaji zinavyofanyika katika kituo cha Uzalishaji Maji Ihelele Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) akielezea shughuli za  uendeshaji zinavyofanyika ndani ya Mamlaka.