MALENGO
     
 

Malengo ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga yamewekwa kwa neno la SMART , kila herufi inawakilishwa na maneno haya  (Specific, Measurable, Attainable, Realistic and Time-bound) yakimaanisha yaliyo maalum, yanayoweza kupimika, yanayoweza kupatikana, kweli na mpaka wa wakati, yakionyesha matokeo au mafanikio. Kila mafanikio yaliyopatikana yanatarajiwa kuiwezesha Mamlaka kutoa huduma ya maji ya jumla ya kutosha; na  hatimaye kuwa Mamlaka bora inayoongoza kusini mwa Jangwa la Sahara katika utoaji wa huduma ya Majisafi na Salama ya Jumla.. Kwa hiyo malengo haya, yanaendana na malengo ya Idara na Sehemu katika utekelezaji na utendaji wa kila mtu ndani ya  Mamlaka  ambayo yatakuwa yakifanyiwa tathmini kwa kuzingatia mfumo wa tahmini ya utendaji kazi kwa kupata mkakati wa utekelezaji wa kila lengo kwa Idara na Sehemu zote. Kimsingi, malengo haya yanatoka kwenye mpango mkakati wa Mamlaka uliopo wa miaka mitano.


Malengo ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga ni:-
i. Kupunguza maambukizi ya VVU au maambukizi mapya ya UKIMWI na kusaidia katika kuboresha huduma.
ii. Kuimarisha utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa kupambanana na rushwa.
iii. Matumizi mazuri ya uzalishaji maji yaliyopo  na kuongeza uwezo wa usambazaji.
iv. Kuboresha utoaji wa huduma bora kwa Wateja..
v. Kuboresha mazingira ya kazi.
vi. Uwezo wa kufanya matengenezo ya mfumo wa uzalishaji na usambazaji maji.
vii. Kuboresha uhifadhi wa chanzo cha maji.
viii. Kuboresha usalama na miundombinu.
ix. Uwezo wa kubeba gharama zote.