MAHUSIANO YA JAMII
     
 

Kwa kuzingatia huduma ya kutoa majisafi na usafi wa mazingira kunaweza tokea migogoro ndani ya jamii katika utekelezaji wa Miradi na majukumu ya kila siku, ambayo inaweza kuwa na athari za kijamii na mazingira. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga itatathmini uhusiano wake kuzingatia jamii kwa mapana yake katika maeneo yote ya huduma. Migogoro ndani ya jamii mara nyingi husababishwa na kutokuwa na uelewa, namna ya kupokea maamuzi yaliyofanywa au kuwa na mtazamo hasi wa jamii kwa shughuli za Mamlaka. Hivyo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga itafanya mchakato wa kuhakiki mashauriano yake na jamii ili kuboresha na kudumisha mahusiano na jamii kwa kuchukua hatua za utekelezaji wa kukuza uelewa wa jamii kwa kupitia, kati ya vitu vingine, mikutano ya hadhara; barua; runinga na mahojiano kwenye redio; kuwasilisha mashuleni; huduma kwenye vilabu na makundi mbalimbali ya kuzingatia kama vile Madiwani na Waandishi; matangazo ya magaazeti, mbao za ukutani ya jamii;maonyesho na kufanya majukumu ya ushirika na jamii.