UTANGULIZI
     
 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority - KASHWASA) iliundwa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 45 la tarehe 23 Februari, 2007, kwa mujibu wa Sheria ya Maji (Cap 272) ya Mwaka 1997, ambayo ilibadilishwa na kuondolewa na Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2019. Jukumu kuu la Mamlaka ni kuzalisha Maji kutoka Ziwa Victoria, kusambaza  na kuuza maji kwa jumla kwa Mamlaka zingine zinazohusika na usambazaji wa maji kwa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.