Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) imeshiriki kikamilifu kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji ya ziwa Victoria kipande cha Tinde -Shelui.

Katika ushiriki huo, KASHWASA imesafirisha watumishi wake hadi Kijiji cha Kizonzo, Shelui Wilaya ya Iramba ambako hafla hiyo inafanyika.

Timu hiyo ya KASHWASA imeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KASHWASA Mha. Joshua Mgeyekwa akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mha. Patrick Nzamba.

Uzinduzi wa Mradi huo unafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan.