Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) leo tarehe 14/8/2023 imeshiriki ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Amos Makala.

Ziara hiyo ilikua ya kutembelea mgodi wa dhahabu wa Ishokela Wilayani Misungwi ambapo KASHWASA ilikua miongoni mwa Taasisi za serikali zilizopata mualiko wa kushiriki ziara hiyo.

Ujumbe wa KASHWASA umeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Eng.Patrick Nzamba.Huu ni muendelezo wa ziara mbalimbali ambazo KASHWASA imekua ikishiriki ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano yake na Serikali.

 

 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Amos Makala (Mwenye shati la mistari ya pundamilia) Akizungumza na vyombo vya habari katika ziara yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kashwasa Mha.Patrick Nzamba (aliyevaa koti jeusi)katika ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.