Mamalaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga(KASHWASA) ilikabithiwa gari aina ya double cabin kwa ajili ya kuimarisha shughuli  mbali mbali za Mamlaka.

Gari hiyo ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA na mwakilishi wa Wizara ya Maji Eng.Edward Tindwa ambaye pia alikuwa msimamizi wa maradi wa Maji Tinde-Shelui.

Gari hii ilikua  inatumika kwenye mradi wa Maji  Tinde-Shelui ambao umekamilika kwa sasa.Kukabidhiwa kwa gari hili itatusaidia sana katika kutekeleza shughuli zake kwa wepesi kwani bado Mamlaka inakabidhiwa na uhaba wa gari kwa ajili ya shughuli zake.