Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) ilijinyakulia tuzo tatu za ubora kutoka EWURA.

 

 Tuzo hizo zilikabidhiwa  Jijini Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KASHWASA Eng. Bashir Mrindoko na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr Philip Mpango.

 

 Tuzo walizotunukiwa KASHWASA ni:

 1.TUZO ya utoaji huduma ya maji safi

 

 2.TUZO ya kudhibiti upotevu wa maji

 

 3.TUZO ya kutekeleza mipango ya Taasisi

Ikiwa ni muendelezo wa Malaka ya majisafi na Usafi  wa Mazingira Kahama Shinyanga kupata tuzo hizi amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hio kuwa tuzo hizi zitasaidia kuongeza wigo mpana kwa wengine kuja kujifunza kwa KASHWASA na kujenga mahusiano mazuri.

 

 Tuzo hizi ni muendelezo wa tuzo kama hizi ambazo KASHWASA imekuwa ikizipata tangu ianze kufanya shughuli zake mwaka 2009.

 

Mwenyekiti wa Bodi KASHWASA Eng.Bashiru Mrindoko na Mkurugenzi Mtendaji Mha.Patrick Nzamba wakipokea tuzo kutoka kwa Mhe.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango katika uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2021/22.

 

Tuzo tatu za Ubora walizojinyakulia KASHWASA.