Kashwasa na Wadau wake wamefanya kikao cha kupata uzoefu wa namna ya uendeshaji. Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Maji CPA Joyce Msiru kutoka Wizara ya Maji ndani ya ukumbi wa mkutano Kashwasa tarehe 31/1/2023.
CPA Joyce Msiru alisisitiza kuundwa kwa Mamlaka moja kubwa ya Simiyu Bulk Water Sanitation (SIBUWASA)ikiwa ni moja ya masharti ya utekelezaji wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa kustahimili mabadiliko ya tabia nchi.
Akiongea katika kikao hicho,CPA Joyce Msiru amezitaka Mamlaka zote za Maji kujua nafasi zao kwa mujibu na vifungu vya sheria ya kanuni za Maji.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji katika kitengo cha Usambazaji Maji Mha. Lydia Joseph aliongeza kuwa kanuni za Maji Water Supply Regulation, 2019 zimeweka Mamlaka za Maji katika makundi manne Kundi AA ni Mamlaka zenye Mtandao unaofika 85% na zinazomudu gharama zote za uendeshaji na matengenezo. Kundi B ni Mamlaka zenye mtandao unaofika 65% zinazomudu gharama zote za uendeshaji na matengenezo. Kundi C ni Mamlaka zenye mtandao unaofika 65% zinazomudu gharama zote za uendeshaji isipokuwa sehemu ya gharama za umeme.