KASHWASA YAPOKEA UGENI KUTOKA CHINA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga ilipokea ugeni kutoka nchini China-Ningbo kuoka kampuni ya Ningbo Water Meters siku ya tarehe 17/7/2023.

Lengo kuu la ziara hio ilikua ni kupata mrejesho juu ya mita za maji ambazo wamekuwa wakiiuzia Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga.

Wakishirikiana na watumishi wa KASHWASA kutoka idara ya Ufundi,Kitengo cha manunuzi,Mahusiano ya umma na Biashara wamerjadili changamoto mabali mbali zinazotokea wakati wa zoezi la usomaji wa mita hizo na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

Ikiwa ni mara yao ya kwanza ugeni huu kutoka nchini China Watumishi hao kutoka kampuni ya Ningbo Wter Meters wameahidi kuendeleza ushirikiano baina ya kampuni hio na KASHWASA.

 

 

 

 

 

 

Wageni kutoka China wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mha.Nzamba na baadhi ya Watumishi kutoka KASHWASA.