KASHWASA ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mha.Patrick Nzamba ilishiriki kikalifu katika kuupokea Mwenge wa Uhuru ndani ya Mkoa wa Shinyanga siku ya tarehe 27/7/2023 ndani ya viwanja vya shule ya Msingi Buganika Halmashauri ya Kisahpu kutoka Mkoa wa Simiyu.

Zoezi hilo liliongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Bw.Abdallah Shaib Kaim pamoja na ujumbe wake ulioambana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Yahya Nwanda na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christ

 

 

Mndeme(kulia)

Aidha,zoezi hilo la kupokelewa kwa Mwenge wa Uhuru lilishirikisha kuweka mawe ya msingi,Kufungua na kukagua jumla ya miradi 41 yenye thamani ya shilingi Billioni 14,027,687,009.20

 Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mndeme alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Utakimbizwa umbali wakilomita

571.5 katika Halmashauri sita (6) za Wilaya ambazo ni Kishapu,Manispaa ya Shinyanga,Halmashauri ya Shinyanga,Manispaa ya Kahama,Msalala na Ushetu.

Pia ameendelea kuwaasa wananchi kuendelea kutunza,kuboresha na kulinda miundombinu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kwani inatumia gharama kubwa katika kufikisha huduma maeneo husika.

  Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru  mwaka 2023 ikiwa ni,”Tunza Mazingira Okoa  vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa jamii na uchumi wa Taifa".      

 

                               

 

Picha ya pamoja ya  Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mha.Patrick Nzamba (katikati) na baadhi ya watumishi wa KASHWASA.

Mkuu wa Wilaya Bi.Johari Samizi Akipokea Mwenge wa Uhuru ndani ya Uwanja wa mpira Kolandoto,Manispaa ya Shinyanga siku ya tarehe 28 Julai 2023.