Naibu katibu mkuu wizara ya Maji Mha.Cyprian Luhemeja alitembelea Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga siku ya tarehe 20/7/2023.Lengo kuu likiwa ni kukagua miradi ya maji,uendeshaji wa Mamlaka za maji na ubora wa utoaji huduma kwa wateja wa Mamlaka hizo.

Katika Ziara hio Mhandisi Luhemeja  alipokelewa na Menejimenti za Tasisi za maji ikiwa ni pamoja na KASHWASA,RUWASA Shinyanga,Maji Bonde,Maabara ya Maji Mkoa wa Shinyanga na KUWASA

Akiongea na Wakurugenzi na Wadau mbali mbali wa Mamlaka za Maji Shinyanga aliwataka kuwa wamoja na kushirikiana katika utendaji kazi ili kupunguza ukubwa wa gharama za uendeshaji.

“Sisi ambao tupo kwenye sekta ya maji tumebarikiwa lakini hatujagundua kuwa tupo kwenye sekta muhimu maana Sekta ya maji ni sekta tajiri na haifi  kwa maana  hio maji ni uhai”.Alisema Mhe.Luhemeja katika kikao cha Watumishi.

Aidha,katika kutekeleza adhima hiyo amehimiza kukutana kwa Viongozi wa Mamlaka za Maji kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya uanzishwaji wa Mamlaka moja kubwa ya maji.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa kwenye ziara yake  ndani ya Mkoa wa Shinyanga alifanya Kikao cha pamoja na Watumishi wote kutoka Mamalak za Maji Mkoa wa Shinyanga.

Katika kikao hicho alipata kutoa usahuri na maelekezo mbali mbali kwa watumishi katika kuhakikisha wanaongeza jitihada katika kazi nan a kujituma ili kuweza kufanikisha lengo la makusanyo yanaongezeka na kukidhi shughuli za uendeshaji katika mamlaka hizo.

“Sisi ambao tupo kwenye sekta ya maji tumebarikiwa lakini hatujagundua kuwa tupo kwenye sekta muhimu maana Sekta ya maji ni sekta tajiri na haifi  kwa maana  hio maji ni uhai”.Alisema Mhe.Luhemeja katika kikao cha Watumishi.

 

Baada ya kikao hicho cha watumishi wote aliendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya majisafi na kutoa maelekezo kwa baadhi ya miradi.