Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga(KASHWASA) imejizolea tuzo tatu za ubora  kutoka EWURA.

Tuzo hizo zimekabidhiwa leo Jijini Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KASHWASA Eng.Bashiru Mrindoko na Mhe.Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe.Dr Philip Mpango.

 

Tuzo walizotunukiwa KASHWASA ni:

1.TUZO ya utoaji huduma ya maji safi

2.TUZO ya kudhibiti upotevu wa maji

3.TUZO ya kutekeleza mipangao ya Taasis

 Tuzo hizi ni muendelezo wa tuzo kama ambazo KASHWASA imekuwa ikizipata tangu ianze kufanya shughuli zake mwaka 2009.

Mwenyekiti wa Bodi KASHWASA Eng.Bashiru Mrindoko na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Eng.Patrick Nzamba wakipokea tuzo kutoka kwa Mhe.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango katika Mkutano wa Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka2021/22.