Piachani ni baadhi ya wanawake wa KASHWASA walioshiriki kwenye sherehe hizo.

 

Baadhi ya wanawake wa KASHWASA wakiwa ofisini kabla ya kuanza safari kuelekea kwenye maadhimisho hayo.

 

Wanawake wa KASHWASA washiriki kikamilifu kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika leo Machi 8,2023 katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa Serikali, na Chama. Maadhimisho hayo yalienda sambamba na utoaji wa mifano ya hundi katika vikundi vya wanawake wajasiriamali na utoaji wa gesi za kupikia. 

Akizungumza Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewataka wanawake mkoani humo kuchangamkia fursa za mikopo asilimia 10 ambazo zinatolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani ili wapate shughuli za kufanya na kuinuka kiuchumi.