Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima leo Alhamisi ameshiriki kwenye zoezi la upandaji miti kwenye chanzo cha maji Ihelele.

Zoezi hilo la upandaji miti liliandaliwa na Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais Mhe.Dkt Philip Mpango.Katika zoezi hilo,jumla ya miti elfu tatu(3000)imepandwa.

Wakati huo huo Mhe. Mkuu wa Mkoa alitembelea Skimu kubwa ya Maji kutoka Ziwa Victoria inayosimamiwa na KASHWASA.

Katika majumuisho ya ziara hiyo.,Mhe. Mkuu wa Mkoa amewapongeza watendaji wakuu na wafanyakazi wote wa Bodi ya bonde la Ziwa Victoria pamoja na KASHWASA kwa kazi nzuri wanazofanya kwenye maeneo yao.

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye chanzo cha Maji Ihelele tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa huu.