Serikali kupitia Wizara ya Maji ipo kwenye mchakato wa kuona uwezekano wa kuanzisha Mamlaka kubwa ya kuzalisha na kusafirisha Maji ya jumla kwenye Mkoa wa Simiyu.

Katika kutekeleza adhima hiyo,Serikali imeunda timu ya watalaam kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya uanzishwaji wa Mamlaka hiyo kubwa ya maji ambayo inapendekezwa iitwe Simiyu Bulk Water Supply and Sanitation Authority(SIBUWASA).

Hayo yamejadiliwa kwenye kikao cha wadau wa sekta ya Maji waliokutana tarehe 31/1/2023 kwenye ukumbi wa KASHWASA kwa lengo la kupata Mchango wa wadau hao juu ya uanzishwaji wa Mamlaka hiyo ya maji.Kikao hicho kimeongozwa na Mkurugenzi Idara ya Usambazaji Maji CPA Joyce Msiru kutoka wizara ya Maji.