Mamlaka ya majisafi na Usafi wa mazingira Kahama Shinyanga(KASHWASA)imekabidhi jumla ya Shilingi1,921,600/= kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Town School Mjini Shinyanga.

Mchango huo umekabidhiwa leo 23/01/2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mha.Patrick Nzamba.

Akipokea Mchango huo,Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Matias Busila ameishukuru KASHWASA kwa mchango huo na ameahidi kwamba fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa choo cha walimu wa Shule yake.

Mchango huo umetokana na ombi la Shule hiyo KASHWASA ambapo waliomba wasaidiwe kujenga choo cha kisasa kwa ajili ya matumizi ya walimu wa shule hiyo.

Mchango huo ni mwendelezo wa michango mbali mbali ambayo KASHWSA imekua ikitoa kwa wadau wake zikiwemo Taasisi za serikali zikiwemo shule za msingi na sekondari.