Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba kushoto, akisaidiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Bw. Alex Mpambije kufungua mfuniko wa chember ya outlet wa tangi la Mabale.

 

Leo (17/06/2022) Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba ametembelea kituo cha uzalishaji maji Ihelele, wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo, alitembelea Chanzo cha maji ghafi (Raw Water), Tangi la Maji Mabale na Eneo la uzalishaji maji na kufanya ukaguzi. Katika ukaguzi huo alibaini mapungufu kadhaa na kutoa maelekezo ya kutatuliwa.

 

Mkurugenzi Mtendaji akifanya kikao na Watumishi wa Kituo cha Uzalishaji Maji Ihelele.