Mradi huo wa tenki lenye ujazo wa lita 500,000 utanufaisha wananchi zaidi ya 14,000 na mifugo yao. Pia utakua mkombozi wa wachimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Mwakitolyo (Shinyanga DC). Mradi huu ni muendelezo wa Serikali ya awamu ya sita ya kumtua ndoo mama kichwani.