Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Veronica A. Kessy ameitunuku Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) cheti cha heshima cha utambuzi wa umahiri katika shughuli za maendeleo kwa jamii mwaka 2021. Tukio hilo lilifanyika tarehe 24/03/2022 Halmashauri ya Misungwi mkoa wa Mwanza katika siku ya wadau wa elimu Wilaya ya Misungwi.