Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mh. Johari Musa Samizi ameipongeza KASHWASA kwa kuendelea kushughulikia tatizo la Maji kwenye Mji wa Ngudu
Mh. Mkuu wa Wilaya ametoa pongezi hizo leo tarehe 2/9/2021 alipofika eneo la Mhalo ampako shughuli za kubadilisha mabomba chakavu kwa nia ya kurejesha haraka huduma ya Maji kwenye Mji wa Ngudu

Eneo la Mhalo ni miongoni mwa maeneo korofi ambalo limekuwa likivujisha Maji (leakage) mara kwa mara kutokana na sehemu kubwa ya eneo hilo kuwa ni mto na mbuga na hivyo kuwalazimu KASHWASA kuchukua uamuzi wa kubadilisha mabomba chakavu katika eneo hilo

Mkuu huyo wa Wilaya amepongeza kasi nzuri ya ubadilishaji wa mabomba inayofanywa na timu ya KASHWASA

Amesema kwamba dhumuni kubwa la ziara yake lilikuwa ni kufika eneo la tukio na kukagua maendeleo ya ubadilishaji wa mabomba na ameonyesha hali ya kuridhishwa na kazi inayofanyika

Katika ziara hiyo, Mh. Mkuu wa Wilaya aliambatana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama na alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA CPA Nicolous Oyier