Uongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu pamoja na Mameneja wa RUWASA Mikoa na Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji zilizopo chini ya RUWASA jana wamefanya ziara katika Zahanati ya Ihelele Wilayani Misungwi.

Mbali na kutembelea Zahanati ya Ihelele, ujumbe huo pia ulitembelea katika Shule ya Msingi ya Ihelele.Ujumbe huo uliongozwa na Mhandisi Elizabeth Kingu ambaye alikuwa amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wameahidi kuwa RUWASA imeguswa na changamoto walizozikuta katika Zahanati na shule hiyo na hivyo wataenda kujipanga kwa ajili ya kuja kutoa msaada katika Zahanati na Shule hiyo.

Zahanati hiyo kwa sasa inatoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka sehemu mbalimbali zilizopo jirani na Ihelele pamoja na wengine kutoka Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita.
Kwa upande wa Shule, kwa sasa shule hiyo inazaidi ya wanafunzi 380 wanaosoma kati ya darasa la kwanza hadi darasa la tano.

Kwa ujumla, shule ya Msingi ya Ihelele mbali na kuasisiwa na KASHWASA lakini hadi sasa KASHWASA bado ni mdau mkubwa ambaye anaendelea kujenga madarasa katika shule hiyo.