Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) juzi tarehe 12 Mei, 2021 ilipokea tuzo kutoka EWURA ya kuwa Mamlaka bora nchini kwa kuthibiti upotevu wa Maji (NRW).

Upokeaji wa Tuzo ya uthibiti wa upotevu wa Maji nchini kwa KASHWASA ni muendelezo wa Tuzo zingine ambazo KASHWASA imekuwa ikizipata miaka ya nyuma mfululizo.

Picha hapo chini inamuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Eng. Joshua Mgeyekwa akikabidhiwa Tuzo hiyo na Naibu Waziri wa Maji Eng. Maryprisca Mahundi huku Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Nadhifa Kemikimba akishududia tukio hilo.