Timu iliyoundwa kwa ajili ya kuandaa Water Safety Plan ya Mamlaka imemaliza kuandaa hatua za awali za uandaaji wa nyaraka hiyo.Zoezi hilo la uandaaji wa nyaraka hiyo linaratibiwa na Maafisa kutoka Wizara ya Maji na linasimamiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Mhandisi Laurence Wasala ambaye pia ni Meneja Ufundi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA).