Mkurugenzi Mkuu (DG) wa RUWASA Eng. Clement Kivegalo hivi karibuni aliongoza ujumbe wa viongozi wa RUWASA pamoja na KASHWASA kwa kuitembelea Jumuiya ya Huduma ya Maji ya PASAMWASH iliyopo Kijiji cha Pandagichiza mjini Shinyanga.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu huyo aliongozana na Mameneja wa RUWASA wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora pamoja na baadhi ya Mameneja wa Wilaya kutoka Mikoa hiyo miwili, pia alikuwemo Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Eng. Joshua Mgeyekwa.                             

Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kwenda kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya hiyo ya Huduma ya Maji pamoja na kuwajengea uwezo na ufahamu wa Masuala mbalimbali yanayohusu utoaji bora wa huduma ya maji kupitia Jumuiya hizo za huduma ya maji.