Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Anthony Sanga ameziagiza Mamlaka za maji hapa nchini kusikiliza kero na malalamiko ya wateja pamoja na zile za watumishi.

Katibu Mkuu ameyatoa maagizo hayo Jijini Mwanza kwenye ukumbi wa Benki Kuu wakati anafungua mafunzo ya siku tatu ya Bodi za Wakurugenzi na Menejimenti za Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kanda ya Ziwa Victoria.
Pia Katibu Mkuu amewaasa Watumishi wote wa Mamlaka za maji nchini kuacha tabia ya kuzizoea kero za wananchi badala yake watumie muda wao mwingi kutatua kero za wananchi.

KASHWASA ni miongoni mwa Mamlaka za maji zinazoshiriki mafunzo hayo ambayo yameanza leo na yanatarajia kumaliIka siku ya jumatano tarehe 7/10/2020