Katika kile kinachoonekana kuendana na kasi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Menejimenti ya KASHWASA mjini Shinyanga imeonyesha mfano halisi wa kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais inayowataka viongozi wote wa Umma kutokaa maofisini badala yake watoke nje kwenda kuwasikiliza wananchi na kutatua changamoto zao.

Menejimenti ya KASHWASA imekuwa kinara kwa utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwani viongozi wake maranyingi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kwa kutembelea maeneo ambayo Mamlaka hiyo inatoa huduma pamoja na kukagua miundombinu yake ya maji.

Staili hii ya utendaji kazi imekuwa na mafanikio makubwa kwa Mamlaka hiyo kwani imekuwa ikiisaidia Mamlaka kupata taarifa mbalimbali kwa uharaka zaidi na pale panapokuwa na changamoto za miundombinu yake Mamlaka hiyo imekuwa ikizibaini na kuchukua hatua za haraka.

Chakufurahisha zaidi ni staili ya kujadiliana na kuchukua hatua za haraka miongoni mwa watendaji pale Mamlaka inapopata changamoto.

Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na watendaji wengine waliopewa dhamana ya kutoa huduma kwa wananchi kwani unasaidia kuwapa hamasa watendaji wa chini na kuwafanya waendelee kuwa na mori ya kufanya kazi zao kwa kujituma.