Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (mwenye suti nyeusi) akiwaongoza wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora  wakiwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kuchukua maji ya Ziwa Victoria kupitia mfereji uliojengwa kitaalamu.

Wadau wa Maji mkoa wa Tabora wamefanya ziara kwenye chanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza ili kujionea na kujifunza namna Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga( Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

 

Chanzo: www.malunde.com