Leo watumishi wa KASHWASA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mha. Joshua Mgeyekwa (mwenye koti na shati la bluu bahari pichani juu) wamepata mafunzo kuhusu moto, magonjwa na maadili kazini katika ukumbi wa Ofisi za Nafrac Shinyanga. Semina hiyo ilihusisha mafunzo ya magonjwa ya Homa ya Ini, UKIMWI na Kisukari. Pichani anaonekana Mtaalam wa mambo ya kuthibiti Moto akionesha namna ya kutumia mtungi wenye maji maalum ya kuzimia moto. Pia watumishia walipata fursa ya kupima Virusi vya Ukimwi na Kisukari kwa hiari.

Daktari akitoa elimu kuhusu magojwa ya Homa ya Ini, UKIMWI na Kisukari.

Mha. Felician Kabigumila akitekeleza kwa vitendo mafunzo ya kuzima moto

Baadhi ya watumishi wa KASHWASA wakisikiliza mafunzo mbalimbali toka kwa wataalam.