Ni tarehe 21/2/2019 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) wakikiri kuisoma Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Utumishi wa Umma mbele ya Mgurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Eng. Joshua Mgeyekwa (aliyesimama mbele) kabla ya kuweka sahihi. Pia walikubaliana na kutambua kwamba masharti yaliyo katika hati hiyo ni ya kimaadili na kisheria na wanawajibika kuyatekeleza. Zifuatazo ni picha zaidi za tukio hilo lililofanyika ofisi kuu za Mamlaka hiyo Shinyanga.