MAHUSINO NA WATEJA
     
 

Lengo la KASHWASA ni kudumisha uhusiano mzuri na wateja. Mambo mengine ni kutoa huduma bora, kuwapa wateja habari juu ya nia zao na kutoa majibu ya mahitaji ya wateja. KASHWASA itahakiki kiwango chake cha mahusiano na wateja; itatambua maeneo na namna ya kuboresha na kudumisha uhusiano mzuri na wateja kupitia:


- Kuweka na kufikia makubaliano ya malengo ya kuwa na huduma bora.
- Kuboresha utendaji kazi katika kuhudumia wateja kwa kushughulikia malalamiko ya wateja.
- Kufikia mahitaji na kupanua huduma kwa maeneo ambayo hayajafikiwa.
- Kuhakikisha uwepo wa mawasiliano ya kutosha na wateja ili kuzuia kutokuelewana; na
- Kuendea kuwa na mpango wa bei nzuri.