HUDUMA KWA WATEJA NA MAWASILIANO
     
 

Kutokana na kwamba wateja wetu ndio sababu ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) kuendelea kuwepo, umuhimu wa huduma kwa wateja katika namna ambayo itakuza uhusiano mzuri na wateja hauwezi kutozingatiwa kwa sababu wateja ndio wadau muhimu wanaoamuru chanzo cha mapato ya KASHWASA.Uwezo wa kusimamia huduma nzuri kwa wateja na kutoa huduma bora ni moja kati ya mali yenye thamani zaidi ambayo wakala wa umma inaweza kuwa nayo.  Raia, viongozi wa jamii na wafanyakazi wanataka na kutarajia huduma kuwa sawa au hata kuzidi viwango vya sasa vilivyowekwa kwa biashara zinazofanya vizuri.