"Maji, Uhai Wako"  
HISTORIA YA KASHWASA

Katika kuadhimisha wiki ya maji nchini na siku ya maji duniani, KASHWASA imetumia wiki hiyo kuboresha miundombinu yake ya maji kwa nia ya kuboresha hali ya upatikanaji maji kwa wateja wake.

Akizungumzia zoezi hilo la uboreshaji wa miundombinu ya maji, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usafirishaji maji wa KASHWASA Eng. Laurence Wasala amesema kwamba zoezi hilo linafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza inayoendelea sasa inahusisha uboreshaji wa chemba zote zilizokuwa na changamoto. 

Ameongeza kwamba hadi kufikia leo tarehe 22/03/2025 ambayo ndio kilele cha wiki ya maji nchini na siku ya maji duniani tayari wameshakamilisha uboreshaji wa chemba tatu kubwa ambazo ni kiungo muhimu kwa wateja wa line za kupeleka maji Shinyanga, Maganzo, Kwimba, Kishapu, Mwadui, Maswa, Kahama, Msalala, Nyangh'wale, Nzega, Uyui, Tabora, Igunga, hadi Shelui Wilayani Iramba. Anasema kwamba uboreshaji wa chemba hizo utaimarisha hali ya utoaji wa huduma ya maji kwa wateja wa maeneo hayo yote. 

Hii ni mara ya kwanza kwa  KASHWASA kuitumia wiki ya maji kwa kuboresha miundombinu yake ya maji hususani chemba na mabomba. Kabla ya hapo KASHWASA imekuwa ikiadhimisha wiki hiyo ya maji kwa kusikiliza na kutatua changamoto za wateja wake.

Copyright © 2025 KASHWASA.