KASHWASA IPO KAZINI KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA WATEJA WA KISHAPU, MAGANZO, MWADUI NA MASWAKASHWASA IPO KAZINI KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA WATEJA WA KISHAPU, MAGANZO, MWADUI NA MASWA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) imeanza awamu nyingine ya zoezi la kuboresha miundombinu yake ya maji kwenye line ya bomba linalopeleka maji kwa wateja wa Maganzo, Mgodi wa Almas wa Mwadui, Kishapu na Maswa.

Akielezea kuhusu maboresho hayo, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usafirishaji maji KASHWASA Eng. Laurence Wasala anasema kwamba zoezi linalofanyika kwa sasa ni muendelezo mwa kazi ya kubadilisha viungio vya GRP ambavyo havifanyi kazi ipasavyo na kufunga viungio vya chuma ambavyo ni imara zaidi.

Mkurugenzi huyo wa Uzalishaji na usafirishaji maji anasema kwamba line hiyo ya maji imekuwa ikisumbua kutokana na mivujo ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikitokea kutokana na uchakavu wa viungio vya GRP ambavyo uwezo wake wa kufanya kazi kulingana na presha ya maji ya line hiyo umekuwa siyo mzuri.

Eng. Wasala anasema kwamba kazi hiyo ya maboresho ambayo inafanyika siyo tu kwamba itaboresha upatikanaji na uhakika wa maji kwa wateja wa line hiyo ya maji bali kutasaidia sana kupunguza upotevu wa maji uliokuwa unatokea wakati wa mivujo hususani kwenye eneo korofi lenye urefu wa km zipatazo 21.

Line ya maji inayofanyiwa maboresho inatokea eneo la Old Shinyanga kwenda kwenye Miji ya Maganzo na Kishapu, Mgodi wa Almas wa Mwadui (WDL) na Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.