Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa maji wa Bukene wenye thamani ya shilingi Bilioni 29.3 katika kijiji cha Uduka Wilaya ya Nzega.
BILIONI 29.3 KUONDOA KERO YA MAJI BUKENE WILAYA YA NZEGA -TABORA.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 29.3 kwa ajili ya kukamilisha upanuzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria kwenda Kata za Bukene ,Mwamala, Itobo ,Isanzu na Ikindwa Wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora.
Hayo yamebainika katika Ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora tarehe 08 Oktoba 2024.
Imeripotiwa kwamba, baada ya kukamilika ujenzi wake, mradi huo utanufaisha wanachi zaidi ya laki tisa kwenye maeneo ambayo mradi huo utatoa huduma.
Kukamilika kwa mradi huo kutaongeza mtandao wa maji ya Ziwa Victoria kwenye Wilaya ya Nzega hususani Jimbo la Bukene ambalo lilikuwa halijafikiwa kabisa na maji ya Ziwa Victoria.
Hadi sasa, ni Majimbo mawili tu ya uchaguzi ya Nzega Mjini na Nzega Vijijini ambayo yalikuwa yamefikiwa na huduma ya maji kutoka Ziwa Viktoria.