Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria  kwenda mji wa Tinde siku ya  tarehe 19/1/2023.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi,amesema Serikali imedhamiria kuboresha na kusogeza huduma ya maji Safi na salama karibu na wananchi.

Ameongeza kuwa maradi huo wa maji ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambayo kwenye Ibara ya (97)inatambua kuwa maji ni Msingi wa uhai kwa binadamu lakini pia  wanyama na mimea yenyewe na ni ingini ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza kuhusu afya Mhe.Mpango amesema kuwa ananmpongeza Rais Dkt.Samia Suluh Hassan katika kutilia mkazo wa huduma muhimu ya maji safi na salama kwa maendeleo ya kijamii katika nchi yetu.

Katika hafla hiyo Dkt.Mpango amwewapongeza pia Wenyeviti na Watendaji wa sekta ya maji kwa usimamimizi mzuri wa maendeleo ya sekta ya maji Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla pia ameahidi kufanya ziara nyingne ndani ya Mkoa wa Shinyanga.