Timu za soka za SHUWASA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga) na KASHWASA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga) zimetoka suluhu ya goli 1 -1 kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika leo (24/6/2022) katika uwanja wa KASHWASA. Magoli ya timu zote yalipatikana kipindi cha kwanza cha mchezo ambao ulitawaliwa na ufundi wa hali ya juu. SHUWASA ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli, kabla ya KASHWASA kusawazisha kwa mkwaju wa penati iliyopigwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wake machachari Dickson Lugonzibwa. SHUWASA ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo.

Mchezo huo ulitiwa nakshi zaidi na jezi maridhawa zilizokuwa zimevaliwa na timu zote mbili. SHUWASA wakiwa na jezi za rangi ya bluu bahari, na KASHWASA wakiwa na jezi za rangi ya machungwa na bluu kama inavyoonekana kwenye picha zifuatazo.